• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Afika mahakamani kushtaki shule iliyofurusha mwanawe mwenye rasta

Afika mahakamani kushtaki shule iliyofurusha mwanawe mwenye rasta

Na Maureen Kakah? 

WAZAZI wa mwanafunzi mwenye rasta wamewasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya shule anakosomea kumtimua.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 alijiunga na shule ya Sekondari ya Olympic kaunti ya Nairobi, wiki iliyopita.Alipelekwa shuleni kama watoto wale wengine waliohitimu kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kupita mtihani wa darasa la nane (KCPE).

Wazazi wa mwanafunzi huyo walilipa karo ya Sh12,000 na alikuwa ameingia darasani kuanza kusoma hisibati na jiografia pamoja na wanafunzi wenzake.

Sasa babake mwanafunzi huyo Jumatatu aliwasilisha kesi katika mahakama kuu akiomba mahakama imshurutishe mwalimu huyo kumruhusu mtoto wake aendelee na masomo.

Pia anaomba bintiye asibaguliwe kwa msingi ya kidini. Anaomba korti iamuru bintiye yuko na haki ya kusoma bila kubaguliwa kwani wao ni wa dini ya Kirastafari.

 

You can share this post!

Polisi washtakiwa kwa kuuuza pombe haramu

Westgate: Korti yasema washukiwa wana kesi ya kujibu

adminleo