Kimataifa

Vyombo vya habari Cameroon vyakatazwa kuzungumzia afya ya Rais Biya

Na MASHIRIKA October 14th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

SERIKALI ya Cameroon imepiga marufuku vyombo vya habari kupeperusha taarifa zozote kuhusu afya ya Rais Paul Biya, kufuatia uvumi kuhusu kifo chake.

Waziri wa Masuala ya Ndani Paul Atanga Nji aliwaambia magavana wa majimbo kwamba taarifa hizi “zimeibua wasiwasi na kuvuruga utulivi miongoni mwa raia wa Cameroon.”

“Kwa hivyo mjadala wowote katika vyombo vya habari kuhusu hali ya afya ya Rais umepigwa marufuku,” akasema.

Waziri Nji alionya kuwa “yeyote atakayevunja agizo hilo atakabiliwa vikali kwa mujibu wa sheria.”

Biya, 91, amesalia mamlakani kwa zaidi ya miongo minne (miaka 43).

Kiongozi huyo hajaonekana hadharani tangu Septemba 8, alipohudhuria mkutano katika ya China na Marais wa Afrika.