• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 3:03 PM
Walioua John F. Kennedy, Robert F. Kennedy, Martin Luther King Jr na Malcon X wachunguzwe upya – Kundi

Walioua John F. Kennedy, Robert F. Kennedy, Martin Luther King Jr na Malcon X wachunguzwe upya – Kundi

MASHIRIKA Na PETER MBURU

KIKUNDI cha watu kutoka nchini Marekani kinataka uchunguzi mpya kuanzishwa kuhusu mauaji ya aliyekuwa Rais wan chi hiyo John F. Kennedy, Robert F. Kennedy, Martin Luther King Jr na Malcon X.

Kupitia ujumbe uliotolewa Jumamosi, kikundi cha The Truth and Reconciliation Committee (TRC) linadai kuwa mpango wa mauaji ya wane hao ulifichwa na serikali, sasa wakitaka faili za uchunguzi kufunguliwa upya ili ukweli upatikane.

“Wakati wa kuadhimisha kifo cha Martin Luther Jr, kikundi cha zaidi ya wakazi 60 wanaotambulika Marekani wanataka bunge kufungua upya uchunguzi kuhusu mauaji ya Rais John F. Kennedy, Malcolm X, Martin Luther King, Jr na seneta Robert F. Kennedy,” ujumbe wao ukasema.

“Ujumbe wa pamoja unalitaka bunge kuunda kamati ya kukagua nakala zote za serikali ambazo zinahusiana na Urais wa Kennedy na mauaji yake kama ilivyoamuliwa katika rekodi za JFK, sharia ya 1992.”

Kikundi hicho aidha kinataka uchunguzi wa umma kuhusu vifo hivyo ili kupata ushahidi wa mashahidi waliopo, wataalam wa kisheria, wanahabari wa upekuzi na wanahistoria, mbali na wanafamilia.

Ujumbe wao ulitolewa Januari 19, siku mbili baada ya kuadhimishwa kwa siku ya kuzaliwa kwa Martin Luther na mbili kabla ya kuadhimishwa kwa sikukuu ya kifo chake.

“Wote hao walikuwa wakijaribu kubadilisha US kutoka vitani, na kuwacha mambo ya silaha na mambo ya Amani,” ukasema ujumbe huo.

“Mauaji yao kwa jumla yalikuwa mateso kwa demokrasia ya Marekani na matokeo yake yanaathiri taifa hili hadi leo.”

Kikundi hicho sasa kinataka mambo ya giza yaliyowahi kutendeka katika taifa hilo kufichuliwa.

Ujumbe wao unahusisha ushahidi kutoka kwa watu waliokesi katika kesi ya John F Kennedy ambapo daktari aliyemfanyia upasuaji akitaka kuokoa maisha yake alisema kuwa mtu aliyefungwa kufuatia mauaji hayo Lee Harvey Oswald, alikuwa akifanya kazi kwa ushirikiano.

Baadhi ya nakala zimedai kuwa mauaji ya Kennedy yalihusisha ushirikiano wa hali ya juu kwenye uongozi wa US na ulitekelezwa na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu sana katika vikosi vya usalama wa taifa hilo.

“Walishirikiana na wahalifu wa hali ya juu kutekeleza uovu huo na baadaye kuficha ukweli,” ujumbe huo ukasema.

Maswali sawa yameibuliwa kwenye mauaji ya Robert F. Kennedy, ambaye alikuwa ameonyesha nia ya kufungua upya uchunguzi dhidi ya kifo cha John, kabla yake kuuawa mnamo 1968.

Kikundi hicho kinasema kuwa umma umenyimwa haki ya kuwapo kwa uwazi katika kesi hizo na idara za usalama za CIA na zingine.

Wananchi wa US sasa wanashauriwa kujiunga na maombi hayo kwa kujisajili na kutia saini nakala za kikundi hicho ili kusukuma bunge kufungua upya uchunguzi wa kesi hizo.

You can share this post!

UTAFITI: Inawachukua wakuu wa kampuni siku 1 kupata...

Siwezi kuiba mamilioni ya mteja wangu, wakili ajitetea

adminleo