Muuguzi aliyetunga mimba mgonjwa mahututi anaswa

NA MASHIRIKA

MUUGUZI wa kiume alikamatwa jimbo la Arizona Jumatano kuhusiana na kisa ambapo mwanamke aliyepoteza fahamu kwa muda mrefu alipata mimba na kujifungua.

Polisi walisema mwanamke huyo wa miaka 29 hakuwa katika hali ya kukubali kufanya ngono, lakini mwezi uliopita alijifungua mtoto mvulana, hali ambayo iliwafanya polisi kuanzisha uchunguzi.

Baada ya uchunguzi, mshukiwa alipimwa na DNA ya mwili wake kupatikana kuwa sawa na ya mtoto aliyezaliwa. Ni hali hii iliyowafanya polisi kumkamata, wakasema.

Mshukiwa anafahamika kama Nathan Sutherland, 36 na sasa anakumbana na mashtaka ya dhuluma za kingono na lingine la kumdhulumu mtu asiyejiweza, mkuu wa polisi eneo la Phoenix Tommy Thompson akaeleza wanahabari.

Habari zinazohusiana na hii