Jamhuri Dei 2024: Ruto aongoza maadhimisho ya miaka 61
RAIS William Ruto anaongoza taifa katika maadhimisho ya Jamhuri Dei 2024, yanayofanyika leo, Alhamisi, Desemba 12 Uhuru Gardens, Nairobi.
Kenya inaadhimisha miaka 61 baada ya kupata uhuru wa kujitawala kama Jamhuri Desemba 12, 1963, miezi sita na siku 11 baada ya kupata uhuru wa ndani kwa ndani kutoka kwa Mbeberu.
Maadhimisho ya Jamhuri hufanyika kila mwaka.
Rais Ruto, tayari ametua katika Bustani ya Uhuru, ambapo alitanguliwa na naibu wake, Prof Kithure Kindiki na Mkuu wa Mawaziri, Musalia Mudavadi.
Dakika chache kabla ya saa nne asubuhi, kiongozi wa nchi alikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na kikosi cha majeshi ya ulinzi ya Kenya (KDF).
Kwenye hotuba yake, anatarajiwa kuainisha sera zake na ajenda za maendeleo kwa taifa.
Rais wa Gambia, Adam Barrow ni kati ya viongozi mashuhuri Barani Afrika ambao wamealikwa kushiriki maadhimisho ya Jamhuri 2024.