• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Aliyemkata shabiki wa Everton usoni asakwa

Aliyemkata shabiki wa Everton usoni asakwa

MASHIRIKA Na PETER MBURU

SHABIKI wa Everton ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kukatwa usoni na mwenzake wa Millwall atatibiwa na aliyekuwa mshindi wa shoo moja ya BBC Dkt Leah Totton, mnamo 2013.

Bw Jay Burns alikuwa amechapisha picha yake mitandaoni, akionyesha kidonda alichopata, baada ya vurugu kuibuka kati ya mashabiki wa timu hizo Jumapili.

Lakini alipoona picha za shabiki huyo, alisema kuwa madaktari wake watamtibu bila malipo, akisema “masikini mwanaume huyu, ni vibaya sana kufanya hivyo kwa uso wa mtu.”

“Ikiwa yeyote anamjua jamaa huyo, tafadhali mwambie azungumze na Dkt Leah Clinics, akipona kidogo, tungependa kumtibu ili kupunguza vidonda na alama bila malipo.”

Jamaa huyo ambaye anaishi Jijini Liverpool aliandika kwenye mtandao wake kuwa “nimehuzunishwa na uso wangu kabisa. Hata siwezi kujiangalia kwenye kioo.”

Katika video inayozunguka mitandaoni, polisi wanaonekana wakiwatawanya mashabiki wanaopigana kabla ya kuanza kwa mechi ya FA, katika uwanja wa New Den.

Mvamizi anaaminika kuwa shabiki wa Millwall.

Polisi walithibitisha kuwa walimpata mwanaume ambaye yuko chini ya miaka 30 akiwa na jeraha la kukatwa usoni, japo hakuna yeyote ambaye amekamatwa.

Baada ya kukatwa, alikimbizwa katika hospitali ya South London ambapo alitibiwa.

Inspekta wa polisi Darren Young alisema kuwa polisi wanachunguza kufahamu waliomtendea mwanaume huyo hivyo, akikashifu kitendo chenyewe.

“Tabia za waliohusika katika kisa hiki ni za kushtua na tutahakikisha tumewatambua,” akasema.

Wakati huo huo, timu ya Millwall iko kwenye hatari ya uwanja wake kufungwa, kufuatia madai kuwa wakati wa mechi hiyo nyimbo za dhuluma za rangi zilikuwa zikiimbwa. Tayari uchunguzi kuhusu madai hayo umeanzishwa.

Kanda ya video inawaonyesha mashabiki wakiimba wimbo wa kudunisha watu fulani.

You can share this post!

Mwigizaji asimulia jinsi amekuwa akikwepa kifo

Sharks yarejea mazoezini kujiandaa kwa mlima wa KPL

adminleo