Uganda ilikuwa nyumbani kiroho kwa Mwanamfalme Aga Khan wa IV
KUTAWAZWA kwa Mwanamfalme Karim Al-Hussaini Aga Khan wa IV kama Imamu wa 49 wa Waislamu wa Shia Ismaili Kampala, mnamo 1957, kuliifanya Uganda kuwa na Imamu kwa mara ya kwanza katika karne ya 14.
Leo, ni wachache tu wanaofahamu msikiti wa Old Kampala, ambapo Aga Khan alitawazwa.Eneo hilo halijavutia umakini wa wengi licha ya kuwa linapatikana katikati ya jiji.
Msikiti huo hata hivyo umevutia umakini wa wengi hivi karibuni kufuatia kifo cha Aga Khan mnamo Februari 4.Sasa ni zaidi ya mahali pa ibada kwa maelfu ya wafuasi wake nchini Uganda; kwa wengi, ndio msingi wa uongozi wake wa kiroho.
Miradi yake ya kiuchumi, kuanzishwa kwa taasisi nyingi ambazo zinaendelea kubadilisha maisha imeathiri mamilioni ya watu kote Uganda, Afrika Mashariki na ulimwengu wakati wa uongozi wake wa miaka 68.
Mnamo Oktoba 9, 2017, serikali ya Uganda ilimkabidhi Mwanamfalme Aga Khan, Tuzo Bora Zaidi ya Pearl of Africa – tuzo ya juu zaidi ya kiraia iliyotolewa kwa wakuu wa nchi na serikali– kwa kutambua mchango wa taasisi ya Uimamu kwa maisha ya Waganda.
Ingawa Aga Khan hakuwa mkuu wa nchi, nafasi yake ilimfanya astahili kupewa tuzo hiyo.
Kulingana na Profesa Mahmood Mamdani, ambaye alitoa mhadhara katika kumbukumbu ya miaka 60 ya Uimamu, kwamba Mwanamfalme Aga Khan ni kiongozi wa kiroho asiye na ubaguzi na anayeheshimika kote ulimwenguni.
Aga Khan alikuwa akiheshimiwa mno Uganda kwani alikuwa na uwezo wa kufunga shirika la kimaendeleo la Aga Khan Development Network (AKDN) ila hakufanya hivyo na shirika hilo likakua kwa kasi japo kupingwa na wengi.
Baadhi ya uwekezaji huu ulikuwa katika uzalishaji wa umeme, kupitia mradi wa umeme wa Bujagali na Kampuni ya West Nile Rural Electrification Company Ltd (Wenreco) na kampuni ya usafiri wa anga ya Air Uganda iliyozinduliwa mwaka 2007 iliyowezesha usafiri kutoka Entebbe hadi maeneo ya Afrika Mashariki.
Wakati bwawa la kuzalisha umeme la 250MW la Bujagali lilipozinduliwa mwaka 2012, liliashiria mwisho wa kipindi kirefu cha Wauganda kukaa gizani.