
Maamuzi ya korti kuhusu mtoto kupata sapoti ya baba au mama. PICHA|HISANI
SWALI: Hujambo shangazi? Baba wa mtoto wangu amekataa kumtunza mtoto licha ya kuwa na uwezo.
Nimemtafuta mara kadhaa bila mafanikio. Naomba ushauri.
JIBU: Mzima, nashukuru. Ikiwa baba wa mtoto wako ana uwezo wa kumtunza lakini amekataa, ni muhimu kuchukua hatua rasmi.
Tafuta msaada wa kisheria kupitia idara ya watoto au shirika la kijamii lililoko karibu. Huyo ni mwanawe na hafai kuhepa majukumu.