• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:10 PM
Sharks kutetea ubingwa wa SportPesa Shield

Sharks kutetea ubingwa wa SportPesa Shield

Na GEOFFREY ANENE

KARIOBANGI Sharks itatetea ubingwa wake wa soka ya SportPesa Shield itakayoanza Machi 1 na kutamatika Juni 1 mwaka 2019.

Sharks iliibuka mshindi wa mwaka 2018 baada ya kuzima mabingwa wa mwaka 2007, 2010 na 2014 Sofapaka 3-2 katika fainali ya kusisimua uwanjani Kasarani mnamo Oktoba 20 mwaka 2018.

“Tutatetea taji letu la SportPesa Shield,” Afisa Mkuu Mtendaji wa Kariobangi Sharks, Lynda Ambiyo ameambia Taifa Leo mnamo Alhamisi.

Klabu 64 wanachama wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) hushiriki mashindano haya ya muondoano ambayo yamekuwa yakifanyika humu nchini tangu mwaka 1956.

Ikitangaza tarehe za makala ya mwaka 2019, FKF imesema kwamba klabu zitakazokuwa zimejiandikisha kufikia Machi 1, 2019 ndizo zitashiriki.

Mshindi wa kombe hili kuzawadiwa Sh2 milioni na pia tiketi ya kuwakilisha Kenya katika soka ya Kombe la Mashirikisho la Afrika (CAF Confederation Cup). Katika Kombe la Mashirikisho la msimu 2018-2019, Sharks ilichabanga Arta Solar7 ya Djibouti kwa jumla ya mabao 9-1 katika awamu ya kuingia raundi ya kwanza kabla ya kubanduliwa nje ya Asante Kotoko ya Ghana kwa jumla ya mabao 2-1 katika raundi ya kwanza.

Matokeo ya mwaka 2018 kutoka raundi ya 16-bora:

Raundi ya 16-bora

Julai 21: Modern Coast Rangers 1-3 Kariobangi Sharks, Friend Zone 0-2 Riverplate, Kenya Police 0(4)-(3)0 Leysa

Julai 22: Vihiga United 1-2 Ulinzi Stars, Tusker 1-0 Bungoma Superstars, Sofapaka 4-1 Western Stima

Julai 25: AFC Leopards 2-1 Mwatate United, Posta Rangers 1-3 Gor Mahia

Robo-fainali

Septemba 1: AFC Leopards 4-1 Kenya Police, Riverplate 1-4 Ulinzi Stars

Septemba 2: Sofapaka 2-1 Tusker, Kariobangi Sharks 4(0)-2(0) Gor Mahia

Nusu-fainali

Septemba 23: AFC Leopards 0-1 Sofapaka, Kariobangi Sharks 4-1 Ulinzi Stars

Fainali

Oktoba 20: Kariobangi Sharks 3-2 Sofapaka

You can share this post!

Kenya yashuka viwango vya FIFA hadi 106

Chokoraa waliosafirishwa Baringo warejeshwa Nakuru

adminleo