Kimataifa

Serikali ya Ufaransa yakana madai inachochea ‘Vita vya 3 vya Dunia’

Na MASHIRIKA May 14th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema kuwa nchi yake haina mpango wowote wa kuchochea Vita vya Tatu vya Dunia kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Katika mahojiano Macron aliahidi kuandaa kura ya maoni huku akieleza malengo yake kwa kipindi kilichosalia cha miaka miwili ya muhula wake madarakani.

Kiongozi huyo aliyeingia madarakani mwaka 2017 akiahidi mabadiliko makubwa, ataondoka madarakani mwaka 2027 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili inayoruhusiwa na katiba.