• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:27 PM
Wauzaji wa nepi feki waachiliwa kwa dhamana

Wauzaji wa nepi feki waachiliwa kwa dhamana

Na RICHARD MUNGUTI

MMILIKI wa wa kampuni ya Imperial Industrial Park Limited Mukhtar Rahemtulla Omar na meneja walishtakiwa kwa kuuza Nepi za watoto feki.

Bw Omar na Bw John Githinji Gichuhi walifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi mkuu mahakama ya Milimani Bi Martha Mutuku wakikabiliwa na mashtaka ya kupatikana na kontena iliyojaa nepi feki.

Mabw Omar na Gichuhi walikanusha mashtaka matatu dhidi yao na kuomba waachiliwe kwa dhamana.

Mahakama ilifahamishwa na kiongozi wa mashtaka Bi Kajuju Kirimi kuwa kesi dhidi ya Bw Omar na Bw Gichuhi itasikizwa kwa pamoja.

Korti ilielezwa washtakiwa walikutwa katika mabohari yanoyomilikiwa na Imperial yaliyoko eneo la Mlolongo, Kaunti ya Machakos akiwa na kontena ikiwa na mabunda 5094 ya nepi feki.

Shtaka lilisema nepi hizo hazikuwa zimewekwa alama ya siku ya kutengenezwana na muda wa kutamatika.

Washtakiwa hao walidaiwa pia walikutwa wakifuta siku ya kutengenezwa kwa Nepi hizo zilijulikanavyo Ezee.

Bi Mutuku aliombwa aamuru kesi hiyo itajwe Feburuari 26 kwa vile Omar ni mgonjwa na anatazamia kusafiri ng’ambo kwa matibabu maalum.

“Sipingi washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana,” alisema Bi Kirimi.

Mahakama iliamuru kila mmoja aachiliwe kwa dhamana ya pesa tasilimu Sh200,000 hadi Februari 28, 2019 kesi itakaposikizwa.

You can share this post!

Murathe si wa hadhi yangu, asema Ruto

Maafisa wa NTSA wanaoshukiwa kuhusika kwa mauaji ya DusitD2...

adminleo