Ndege yaanguka msituni Urusi na kuua abiria wote 50
MOSCOW, URUSI
NDEGE ya Urusi iliyokuwa na abiria 50 Alhamisi, Julai 24, 2025 ilianguka Mashariki mwa nchi hiyo na ilihofiwa kuwa abiria wote hao.
Idara ya Kupambana na Majanga ilithibitisha ajali hiyo ambayo imezua wimbi la huzuni katika nchi hiyo.
Ndege hiyo ilitengenezwa enzi za Usovieti na ilikuwa imetumika kwa karibu miaka 50.
Kufikia wakati wa kupeperusha taarifa hii, waokoaji bado walikuwa wakielekea eneo hilo kutoa msaada.
Video iliyopigwa ndani ya helikopta iliyokuwa angani ilionyesha ndege hiyo ilianguka msituni na moshi ulikuwa ukitokea mahali iliangukia.
Taarifa ziliarifu kuwa ndege hiyo ilimilikiwa na Shirika la Ndege la Serbia linalofahamika kama Angara.
Ndege yenyewe ilitengenezwa mnamo 1976 na ilikuwa ikisimamiwa na kampuni ya Aeroflot kabla kuporomoka kwa Muungano wa Usovieti mnamo 1991.
Serikali ya Urusi imesema kuwa ilikuwa ikitoka jiji la Blagoveshchensk hadi Tynda, eneo la Amur kwenye mpaka wa Urusi na China.
Kulikuwa na abiria 45 wakiwemo watoto na marubani sita ndani ya ndege hiyo kwa mujibu wa serikali ya eneo la Vasily Orlov ambako ilianguka.
Hata hivyo, serikali kuu iliweka idadi ya abiria kuwa 42.
Pia ilisema kuwa ilikuwa imebuni tume kushirikiana na maafisa wa usalama na uchukuzi kuchunguza kiini cha ajali hiyo na pia kutolewa kwa usaidizi wowote kwa familia za walioangamia.
Rais Vladimir Putin alifahamishwa kuhusu ajali hiyo na alitarajia kuzungumzia taifa kuihusu.