• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
Mwalimu amuua mumewe kwa kumnyima uroda

Mwalimu amuua mumewe kwa kumnyima uroda

RICHARD MUNGUTI Na DAILY MONITOR

KALIRO, UGANDA

MWALIMU wa shule ya msingi aliyekuwa na uchu wa kuburidishwa kitandani na mume wake, alitenda kisa cha kiajabu alipomuua kwa kukataa kumlisha uroda.

Polisi walioitwa kuondoa maiti ya mumewe aliyekaidi matakwa ya mkewe amwondolee kiu ya muda mrefu ya mapenzi, walisema mwalimu huyo alitumia kisu anachokatia kitunguu kumuua baba watoto.

Mwanamke huyo aliyetambuliwa na Polisi kwa jina Harriet Nambi mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Nakiyanja kilichoko katika baraza la miji wa Kaliro nchini Uganda alimfuma mumewe Musa Batera mwenye umri wa miaka 25 kifuani na kumsafirisha ahera.

Kwa mujibu wa Polisi marehemu alikuwa amekataa kujamiiana na mkewe kwa vile alikuwa amejifungua yapata miezi miwili iliyopita kwa njia ya kufanyiwa upasuaji (caesarean).

Hadi kifo chake, Batera, ambaye ni mume wa wake watatu alikuwa mwenyekiti wa chama che wenye piki piki almaarufu Boda Boda katika mji wa Kaliro tangu 2011. Nambi mwalimu katika shule moja ya msingi mjini Kaliro.

Bi Hasifa Babriye ambaye ni jirani yao alifichua mke huyo na mumewe walikuwa wameanza kufarakana baada ya Nambi kumlaumu mumewe kwa kutompa haki yake ya ndoa.

Mzozo baina ya wawili hao ulikuwa umeanza siku tatu kabla ya Nambi kumdunga kisu cha kifuani..

“Nambi alinieleza mumewe alikuwa amekataa kumtimizia haja zake ilhali alikuwa na kiu kikuu. Nilimshauri asubiri apone kwa vile alikuwa amefanyiwa upasuaji miezi miwili iliyopita,” Babriye alidokeza

Aliongeza, “Nilimshauri ampe mume muda lakini alikataa akisema lazima atamdhuru. Mumewe aliporejea kwa nyumba walikorofishana kisha akamdunga kisu cha mauti.”

Kwa mujibu wa wakazi, Nambi alimshawishi mumewe kuingia chumbani mwao na punde ugomvi ukaanza kisha vita vikazuka.

Afisa mkuu wa Polisi Wilaya ya Kaliro Bw Joseph Kihamba, alithibitisha kisa hicho na kuongeza , “ Nambi ametiwa nguvuni na atafunguliwa mashtaka ya mauaji.”

Bw Kihamba amewashauri wanandoa wasuluhishe tofauti zao kwa njia ya amani na kuwashirikisha watu wa familia zao.

Pia aliwasihi wanandoa wawasiliane na afisi za kijamii badala ya kuchukua sheria mikononi.

Afisa huyo alisema mwalimu huyo angelisubiri tu kwa vile alikuwa amejifungua hivi majuzi na hajapona kidonda.

“Kile mwanawake huyo mwenzangu alifanya ni makosa. Alikuwa amejifungua hivi majuzi na alikuwa amekazana atimiziwe mahitaji yake ya kijamii ilhali madaktari ushauri wanawake wasubiri hadi miezi sita ipite baada ya kujifungua ndipo wawe wamepona. Hakuwa tayari kwa mapenzi,” alisema Jamila Nangiya, mkazi wa Kalirobaada ya kupokea habari hizo za kushtua.

Polisi waliipeana maiti ya Batera kwa familia yake wakaizike huku uchunguzi ukiendelea.

You can share this post!

Wahuni wanataka kichwa na viungo vya mwili wangu –...

Maafisa wa polisi mashakani kwa kugeuza gari la serikali...

adminleo