Habari za Kitaifa

Raila ajiunga na orodha ya waliokosa urais licha ya kupendwa

Na DAVID MWERE October 18th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

KATIKA kifo chake, aliyekuwa waziri mkuu Raila Amolo Odinga, na kiongozi wa ODM, amejiunga na orodha ya viongozi wa Afrika ambao, licha ya umaarufu wao mkubwa na nguvu ya kisiasa, hawakufaulu kutwaa uongozi wa mataifa yao.

Hawa ni watu waliobaki katika kumbukumbu za umma kwa misimamo yao na kupigania haki, ingawa hawakuingia Ikulu.

Miongoni mwa majina haya ni Etienne Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambaye, licha ya ushawishi wake, hakuwahi kuwa rais. Viongozi wengine ni John Garang wa Sudan Kusini, Patrice Lumumba wa DRC, na Moshood Abiola na Obafemi Awolowo wa Nigeria ambao walivuma katika siasa za nchi zao lakini hawakushinda urais..

Profesa Herman Manyora, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alisema Raila ataandikwa katika historia kama Rais ambaye Wakenya hawakuwahi kumpata. Mapokezi ya mwili wake yalionyesha alivyopendwa na watu, zaidi ya yale yaliyoshuhudiwa wakati wa kifo cha Moi na Kibaki.”

Seneta Enock Wambua wa Kitui alisema ni huzuni Raila hakuwahi kuwa rais.