Watu wawili wafa baada ya ndege kutumbukia baharini
WATU wawili walifariki Jumatatu baada ya ndege moja ya mizigo kutumbukia baharini baada ya kupoteza mwelekeo ikitua katika Uwanja wa Kimataifa wa Hong Kong.
Ndege hiyo nambari EK9788 ya Shirika la Emirates ilikuwa ikiwasili kutoka Dubai mwendo wa saa tisa alfajiri ilipopoteza mwelekeo na kugongana na gari la doria.
Watu wawili waliokuwa ndani ya gari hilo ndio walikufa ilhali wahudumu wanne waliokuwa kwenye ndege hiyo walinusurika.
Ajali hiyo ni mojawapo ya mbaya ya ndege ndani ya miaka mingi katika uwanja huo wa kimataifa wa Hong Kong. Uwanja huo, hata hivyo, uko na rekodi nzuri ya usalama.
Maafisa wa utawala wameanzisha uchunguzi kufuatia ajali hiyo huku maswali yakiulizwa kuhusu mkondo ambao ndege hiyo ulifuatwa baada ya kutua.