Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Huwa tunakosana kila mara, ndoa itadumu?

Wanandoa wanaofarakana. Picha|Maktaba
Swali: Nina umri wa miaka 21 na nimekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke fulani.
Tumekosana na kurudiana mara kadhaa. Je, hizo ni dalili kuwa uhusiano wetu hauwezi kudumu?
Jawabu: Kwangu mimi, hizo ni dalili kuwa mapenzi yenu ni ya dhati na yatadumu. Kama si mapenzi mngekuwa mmeachana. Kukosana ni jambo la kawaida hata kwa walio katika ndoa. Lakini palipo na mapenzi pia pana msamaha. Ondoa hofu.