Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Ataka tuwe na uhusiano wa pembeni ila mkewe ni rafiki yangu mkubwa

Na SHANGAZI November 6th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Nina umri wa miaka 33. Kuna mwanamume rafiki yangu ambaye ameoa na anataka tuwe na uhusiano wa pembeni. Nampenda lakini mke wake ananijua na nahofia atagundua. Waonaje?

Jibu: Mpango wa kando na waume au wake wa wenyewe ni wa muda tu tena ni hatari. Kuna hatari ya mke wake kugundua na hujui atachukua hatua gani. Wewe bado ni mchanga. Kwa nini usitafute wako?

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO