Shangazi Akujibu

Nina mpango ila kumbe naye mke ananicheza!

Na SHANGAZI November 19th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Shikamoo shangazi? Nimeoa na tuna watoto. Nimekuwa na mpenzi wa pembeni kwa mwaka mmoja. Nimegundua mke wangu pia ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine. Je, amegundua siri yangu na kuamua kulipiza kisasi?

Jibu: Mimi sijui. Ninachojua ni kwamba mnapoteza wakati na itakuwa muhimu kuweka mambo wazi ili mjue hatima ya ndoa yenu. Itabidi muongee wazi kuhusu mipango yenu ya kando ili mjue hatima ya ndoa yenu.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO