Habari

Ni kibarua kigumu kwa Ruto baada ya Raila kufariki – TIFA

Na CECIL ODONGO December 24th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

WAKENYA wengi waamini kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga kimesababisha uwezekano wa Rais William Ruto kuchaguliwa tena kuwa kugumu zaidi, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Tifa.

Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 41 ya Wakenya wanasema itakuwa vigumu zaidi kwa Rais kushinda bila Raila ambaye aliaga dunia mnamo Oktoba 15.

Ni asilimia 30 pekee ya Wakenya wanahisi kwamba itakuwa rahisi sana kwa Rais Ruto kupata muhula mwingine bila Raila.

Asilimia 18 nao wanasema Raila awe au asiwe hakuna tofauti zozote katika kuchaguliwa au kutochaguliwa kwa Rais Ruto.

Asilimia 10 nao walisema hawana ufahamu wowote kuhusu suala hilo.