• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
ODM, ANC kwenye mvutano wa ni nani ateuliwe naibu gavana Nyamira

ODM, ANC kwenye mvutano wa ni nani ateuliwe naibu gavana Nyamira

RUTH MBULA na CHARLES WASONGA

VUTA nikuvute katika Kaunti ya Nyamira kuhusu uteuzi wa Naibu Gavana itaendelea kwa muda baada ya ODM kuendelea kushinikiza chaguo lake ndiye ateuliwe huku Gavana Amos Nyaribo akisisitiza kumteua James Gesami.

Kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, Jumatano alimtetea Gavana Nyaribo akikashifu ODM kwa kuhujumu uongozi wa Nyaribo kwa kumwekea vikwazo.

“Kama chama cha ANC tunapinga njama zinazoendelezwa na watu hao ambao wanataka kuvuruga uongozi wa Bw Nyaribo kwa kumsukumia kibarakala wao eti ndiye ateuliwe kama naibu wake,” Bw Mudavadi akasema kwenye mahojiano katika kituo cha redio cha Egesa FM kinachopeperusha matangazo kwa lugha ya Ekegusii.

Kwa mara ya pili sasa, ODM imependekeza Bw Charles Rigoro ateuliwa chini ya kile ODM inasema ni mkataba uliokuwepo kwamba ODM na ANC walifaa kugawana uongozi wa Kaunti ya Nyamira kwa usawa.

“Ilivyoelezwa katika barua yetu ya Januari 20, 2021, iliyotiwa saini na mwenyekiti John Mbadi, chama kimependekeza Bw Charles Rigoro ateuliwe kwa wadhifa wa Naibu Gavana,” ikasema barua hiyo iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna na kutumwa kwa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kaunti ya Nyamira Duke Masira.

You can share this post!

Man-United, Man-City na Chelsea kusambaratisha Dortmund...

Kampuni yaomba serikali kupunguza gharama ya umeme