Kimataifa

Muhoozi akana madai kuwa jeshi lilishambulia mke wa Bobi Wine: ‘Hatupigi wanawake, mtu tunataka ni Kabobi’

Na REUTERS January 27th, 2026 Kusoma ni dakika: 1

KAMPALA, UGANDA

JENERALI Muhoozi Kainerugaba amekana madai kwamba wanajeshi walimshambulia mke wa kiongozi wa upinzani Bobi Wine.

Wine anadai kuwa wanajeshi walivamia nyumba yake usiku wa kuamkia Jumamosi katika kitongoji cha Magere jijini Kampala, na kisha kushambulia wafanyakazi na mkewe, Barbara Kyagulanyi.

Wine, ambaye amekuwa mafichoni kufuatia uchaguzi wa urais alisema hakuwepo nyumbani wakati huo.

Kainerugaba alipuuza madai hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X, akisema jeshi haliwezi kuwashambulia wanawake.

Wine amevishutumu vikosi vya usalama Uganda kwa unyanyasaji tangu uchaguzi wa rais wa Januari 15, ambao Rais Museveni alishinda kwa asilimia 71.6 ya kura.

Mamia ya wafuasi wa NUP walikamatwa wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi huku uongozi wa chama hicho ukisema ilikuwa njia ya kuwaingiza uoga.

Wine ambaye yuko machifoni, alidai kuwa uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu na akatoa wito kwa Umoja wa Afrika uzungumzie mauaji na ukandamizaji wa haki unaoendelea Uganda.