Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Mke amebadilika, anachelewa sana kazini

Na SHANGAZI February 5th, 2026 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Hujambo shangazi? Mke wangu meajiriwa. Siku za hivi majuzi ameanza kuchelewa sana kazini na nikimuuliza husema kazi imekuwa nyingi. Ninashuku bosi wake anamtaka ingawa sina ushahidi. Nishauri.

Jibu: Mwajiriwa anatarajiwa kufanya kazi kulingana na maagizo ya mkubwa wake. Sijui ni kwa nini huamini kuwa mke wako anachelewa kwa sababu ya kazi. Pili, kama ni mwaminifu kwako, huna sababu ya kuwa na wasiwasi.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO