• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 4:25 PM
Ufisadi: Raila atofautiana vikali na kauli ya Waititu

Ufisadi: Raila atofautiana vikali na kauli ya Waititu

Na NDUNGU GACHANE

KIONGOZI wa ODM, Raila Odinga jana alimkemea vikali Gavana Ferdinand Waititu wa Kiambu kwa kuhimiza Serikali ipunguze kasi ya kupambana na ufisadi.

Akizungumza wakati wa mazishi ya mfanyibiashara Thayu Kamau katika Kaunti ya Murang’a, Bw Waititu alikuwa amesema vita hivyo havifai kuwa kali sana kwa

“Tunafaa kuwa waangalifu kwa ajili ya watu wetu wanaoishi Rift Valley kwani huenda wakaathirika ikiwa watu wenye ushawishi katika baadhi ya jamii watakabiliwa kwenye vita dhidi ya ufisadi,” akasema Bw Waititu.

Hata hivyo, aliposimama kuzungumza, Bw Odinga alimpuzilia mbali Gavana Waititu akimwambia Wakenya hawatakubali kutishwa na yeyote kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Alisema makabila yote ya Kenya yana haki sawa za uhuru na kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine.

“Bw Waititu, usiwe na hofu wala kutishwa. Hatutatishika na vitisho kama hivyo katika kupiga vita ufisadi. Lazima tukae ngangari na kuwapeleka wezi wote gerezani,” akasema Bw Odinga.

Rais Kenyatta alimpuzilia mbali Bw Waititu akisisitiza kuwa watu wenye ushawishi watakamatwa na kushtakiwa kuhusiana na ufisadi

Rais aliwashtumu viongozi ambao alisema wanazurura kote nchini wakipiga kelele zisizo na uhumimu, akiongeza kuwa watakamatwa karibuni.

Rais alisema tamaa ya kupata utajiri kwa haraka ndiyo inayosababisha ongezeko la visa vya maafisa wa serikali kujihusisha na wizi wa mali ya umma.

Aliwataka Wakenya, katika tabaka zote za jamii, kuishi maisha ya uadilifu na kutafuta utajiri kwa njia halali kwa kufanya kazi kwa bidii.

“Hatutafika pale tunapotarajia kufika kama taifa iwapo hatutaacha fikra hizo za kujitajirisha haraka,” akasema Rais.

Kiongozi wa taifa alitoa wito kwa Wakenya kuungana katika vita dhidi ya ufisadi kwa sababu unahatarisha ustawi wa taifa.

“Hatuna lengine la kufanya ila kupambana na ufisadi kwa sababu Wakenya wanahitaji barabara, hospitali na ajira. Ushuru tunaotoza Wakenya sharti utumikie umma,” akasema Rais.

Habari za ziada na PSCU






You can share this post!

Uhuru, Ruto wagongana

Gor kuelekea Misri baada ya mechi ya CAF nchini Algeria

adminleo