AFYA: Kuandaa juisi tamu ya tikitimaji
Na MARGARET MAINA
TIKITIMAJI lina manufaa kadhaa mwilini mwa binadamu.
- Asilimia 92 yake ni maji
- Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
- Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili
- Huponya majeraha
- Hukinga uharibifu wa seli
- Huboresha afya ya meno na fizi
- Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vyema
- Hubadilisha protini kuwa nishati
- Chanzo cha madini ya potassium
- Husaidia kushusha Shinikizo la Damu
- Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
- Huondoa sumu mwilini
Muda wa kuandaa: Dakika 15
Idadi ya wanywaji: 4
Vinavyohitajika
- tikitimaji 2
- juisi ya limau nusu kikombe
- asali
- majani ya Mint
- vipande vya barafu
Maelekezo
Katakata tikitimaji katika vipande vidogovidogo, menya ngozi na unaweza kutoa mbegu ukipenda.
Chukua vipande hivyo; saga na juisi ya limau pamoja kwenye blenda.
Baada ya kusaga, ichuje katika chujio safi au ukipenda iache ikiwa nzito.
Ukishafanya hivyo, weka ice cubes pamoja na majani ya mint katika jagi kisha mimina juisi katika jagi lako lenye barafu na mint.
Ukipenda, mimina asali kwenye mchanganyiko wa juisi na ukoroge ichanganyike.
Mimina kwenye glasi na ufurahie kinywaji chako.