• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 11:28 AM
Droo ya SportPesa Shield yatangazwa

Droo ya SportPesa Shield yatangazwa

Na GEOFFREY ANENE

DROO ya soka ya SportPesa Shield ambayo mechi zitasakatwa kutoka Machi 16 hadi Juni 1, imefanywa, huku mabingwa watetezi Kariobangi Sharks wakikutanishwa na Elim katika mechi yao ya raundi ya 32-bora.

Gor Mahia, ambayo inashikilia rekodi ya mataji mengi ya kombe hili la rais wa Shirikisho la Soka la Kenya, italimana na Kenpoly nao mahasimu wao wa tangu jadi AFC Leopards watavaana na Transfoc.

Klabu tisa pekee kutoka Ligi Kuu ndizo zimeingia makala ya mwaka huu. Mbali na Gor, Leopards na Sharks, klbu zingine kutoka Ligi Kuu ni Western Stima, Bandari, Tusker, Ulinzi Stars, Sofapaka na KCB.

Mathare United, SoNy Sugar, Kakamega Homeboyz, Nzoia Sugar, Zoo, Posta Rangers, Chemelil Sugar, Vihiga United na Mount Kenya United kutoka Ligi Kuu hazikuingia mashindano haya ambayo mshindi kuzawadiwa Sh2 milioni na kujishindia tiketi ya kuwakilisha Kenya katika Kombe la Mashirikisho la Bara Afrika (CAF Confederation Cup).

Sharks ilichapa Sofapaka 3-2 katika fainali ya mwaka 2018 na kuwakilisha Kenya katika Kombe la Mashirikisho. Ilibwaga Arta Solar7 ya Djibouti kwa jumla ya mabao 9-1 katika awamu ya kuingia raundi ya kwanza kabla ya kubanduliwa nje na Asante Kotoko ya Ghana katika raundi ya kwanza kwa jumla ya mabao 2-1.

Droo ya raundi ya 32-bora:

Fortune Sacco na Wazito

Uprising na Western Stima

Kenpoly na Gor Mahia

Kayo na Bandari

Congo Boys na Kenya Police

Emmausians na Mwatate United

Naivas na Tusker

SS Asad na Ulinzi Stars

Bungoma Super Stars na Sofapaka

Transfoc na AFC Leopards

Muranga Seal na Kisumu All Stars

Elim na Kariobangi Sharks

Trans Mara Sugar na Bidco United

Dero na FC Talanta

Vihiga Sportiff na Ushuru

Sindo United na KCB

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Vikwazo vinavyokabili Kiswahili...

BAHATI YA VAR: Manchester United wapigana kufa kupona hadi...

adminleo