Matokeo mseto Kenya ikianza Olimpiki kwa walemavu

Na GEOFFREY ANENE

KENYA ilianza mashindano ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu kwa kuandikisha matokeo mseto jijini Abu Dhabi katika nchi ya Milki za Kiarabu.

Mashindano haya yanaleta pamoja zaidi ya mataifa 170.

Mpira wa vikapu: Kenya ilianza mpira wa vikapu kwa kishindo. Ilicharaza Algeria 8-0, Chinese Taipei 16-11, Nigeria 8-2 na Luxembourg 9-8 mnamo Machi 14. Hata hivyo, Wakenya hawakuwa nan a lao katika mechi tatu zilizozfuata ambapo walililmwa na Urusi 11-4, Milki za Kiarabu 20-4 na Ivory Coast 7-6. Mechi hizi pia zilisakatwa Machi 14. Kenya inawakilishwa katika fani hii na wachezaji George Gichiri, Victor Lijembe, Innocent Wafula, Daniel Wanjala, Joshua Omondi, Kimanthi Mbatha, Jack Otiende, James Okal na Douglas Omollo.

Soka: Timu ya Kenya ilinyamazisha Marekani 3-2 katika mechi kali. Wanasoka wa Kenya ni Amos Mulandi, Anthony Thomas, Boniface Kimeu, Daniel Mutiso, Francis Gitau, Gifty Bahati, Jacob Mutisya, Januaries Mwendwa, Josephat Melika, Kennedy Tama, Nahshon Kyalo, David Nzoika, Peter Ndeti, Pius Mutunga, Shadrack Nzioka na Shealtiel Muthoka.

Kenya na Marekani soka. Picha/ Hisani

Voliboli ya ufukweni: Timu ya Kenya ya wanaume inayojumuisha wachezaji Collins Kiplimo, Daniel Kiptoo, Dennis Kiptum, Hudson Kipchumba, Nicholas Korir na Wilson Kirwa ilipepeta Iraq, Uruguay na Finland mnamo Machi 14.

Voliboli: Timu ya Kenya ya wanawake ilizamisha Jamaica na Serbia kwa seti za kufanana za 2-0 Machi 13. Wachezaji wa Kenya hapa ni Beatrice Bilo, Branice Juma, Christine Mukwe, Dolphine Adhiambo, Leah Achieng’, Lorine Ochieng’, Lorine Madoyi, Mary Ajwang’, Purity Akinyi na Rhoda Kakai.

Handiboli: Kenya ililemea Kuwait 11-2 katika mechi yake ya ufunguzi Machi 12.

Kikosi chote cha Kenya ni cha wanamichezo 71.

Wanashiriki soka, mpira wa vikapu, voliboli, voliboli ya ufukweni, handiboli, riadha, ‘bocce’, kuendesha baiskeli, gofu, kuogelea kwenye bwawa na kuogelea katika mto, ziwa ama bahari (Open Water Swimming).

Habari zinazohusiana na hii