• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Wafisadi wote Kenya wanyongwe, mbunge apendekeza

Wafisadi wote Kenya wanyongwe, mbunge apendekeza

Na LAWRENCE ONGARO

MBUNGE wa Thika Mjini Mhandisi Patrick Wainaina, amesema ufisadi umefika kiwango cha kustisha nchini na hivyo serikali inafaa kufuata mfano wa mataifa ya bara Asia ambapo wafisadi hunyongwa.

“Kwa nchi za uarabuni ufisadi na wizi ni kama ndoto kwa sababu kule ukipatikana kuwa mwizi unakatwa mikono au kunyongwa na kwa hivyo watu wengi wamefuata mwito wa kuwa wazalendo kamili,” alisema Bw Wainaina.

“Serikali inastahili kupambana na ufisadi vilivyo bila kujali mtu yeyote yule katika nyadhifa kubwa.”

Aliyasema hayo katika chuo cha walimu cha St John Kilimambogo, Thika Mashariki, alipokuwa mgeni wa heshima wakati wa kufuzu kwa wahitimu wa ualimu wapatao 490.

Alisema dunia ya sasa ina ushindani mkali na kwa hivyo kila mmoja sharti awe na ubunifu wa kipekee, na zimwi la ufisadi litalemaza kila sekta ikiwa hatua haitachukuliwa.

Alitaka ardhi ya Delmonte ya ekari 635 iliyopewa Kaunti ya Kiambu ifanyie maendeleo ikatwe kipande fulani.

 

You can share this post!

Ulinzi na Sofapaka zatupwa nje ya SportPesa Shield

Mamilioni kwa Jepkosgei baada ya kuwika New York City Half...

adminleo