• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Jina la Mutyambai lawasilishwa bungeni

Jina la Mutyambai lawasilishwa bungeni

Na CHARLES WASONGA

IKULU Jumanne iliwasilisha rasmi bungeni jina la Bw Hilary Mutyambai ambaye amependekezwa kuwa Inspekta Jenerali mpya wa Polisi.

Bw Mutyambai ambaye ni afisa wa Shirika la Kitaifa la Ujususi (NIS) atapigwa msasa wiki ijayo mbele ya kamati ya pamoja ya Usalama ya bunge la kitaifa na ile ya Seneti kuhusu Usalama na Maswala ya Kigeni.

Endapo uteuzi wake utaidhinishwa na bunge Bw Mutyambai atachukua nafasi ya Bw Joseph Boinnet ambaye alistaafu rasmi wiki iliyopita.

Katika mabadiliko hayo, Rais Kenyatta alimteua Bw Boinnet kuwa Waziri Msaidizi wa Utalii, cheo ambacho kimekuwa wazi tangu Agosti 2018.

Bunge la kitaifa linatarajiwa kuenda likizo fupi mnamo Machi 28. Hii ina maana kuwa mnamo Aprili 2 wakati ambapo kamati hiyo itatarajiwa kuwasilisha ripoti yake katika mabunge yote mawili, wabunge watakuwa wangali likizoni. Hii ina maana kuwa huenda uteuzi rasmi wa Bw Mutyambai na Rais Kenyatta ukacheleweshwa.

Ikiwa bunge litafeli kupitisha au kukataa jina la mteule ndani ya muda uliowekwa, siku 21, Sheria kuhusu Ukaguzi na Uidhinishwaji wa Wateule wa Nyadhifa za Umma inasema kuwa mteule mhusika atachukuliwa kuwa ameidhinishwa kwa wadhifa aliyependekezewa.

Hii ndio maana Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi aliitaka Kamati inayoratibu Shughuli za Bunge (HBC) kupanga upya kalenda ya bunge ili kutoa muda kwa zoezi hilo kukamilishwa kabla ya wabunge kwenda likizo. Hii ina maana kuwa likizo hiyo fupi itaahirishwa.

“Nitailiza kamati ya HBC kutoa mwelekeo kuhusu kalenda ya Bunge kuhakikisha kuwa shughuli hiyo inakamilishwa ndani ya muda unakubalika kisheria,” akasema baada ya kusoma barua kutoka Ikulu.

Hata hivyo, Bw Muturi alisema shughuli hiyo ya kumpiga msasa Bw Mutyambai itasimamiwa

Kabla ya zoezi hilo kuanza, bunge litatoa tangazo kwa umma mnamo Machi 21, kuwataka kuwasilisha maoni, mapendekezo au pingamizi zozote kuhusu ufaafu kwa Bw Mutyambai kwa wadhifa wa Inspekta Jenerali wa Polisi.

Katiba na Sheria ya Sheria ya Huduma za Polisi zinasema kuwa Inspekta Jenerali atateuliwa na Rais kuidhinishwa na Bunge.

You can share this post!

Nitaangika glovu Porto nikigonga miaka 40 – Casillas

NJAA: Chifu matatani kwa kufichua vifo

adminleo