• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 11:34 AM
Wendawazimu wamejaa hospitalini kutokana na uvutaji bangi – Daktari

Wendawazimu wamejaa hospitalini kutokana na uvutaji bangi – Daktari

Na NDUNGU GACHANE

MTAALAMU wa kutibu maradhi ya kiakili amesema matumizi ya bangi miongoni mwa vijana ndicho kichocheo kikubwa cha kuongezeka kwa idadi ya wendawazimu wanaolazwa katika hospitali ya kaunti ya Murang’a.

Bi Angela Muthoni ambaye ni daktari hospitalini humo, amesema vijana 300, wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule za upili hulazwa kila mwezi kwa kukumbwa na maradhi ya kiakili.

Kulingana na Bi Muthoni, matumizi ya dawa ya kulevya aina ya kuber na bangi yamechangia vijana wengi kugeuka wendawazimu na baadhi yao kujitia kitanzi katika mazingira ya kutatanisha.

Mtaalamu huyo sasa anapendekeza vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya viendeshwe shuleni na katika taasisi za masomo ambako walanguzi wa dawa hizo wamekita kambi usiku na mchana.

Wiki jana, shirika la NACADA lilieleza hofu kutokana na kukithiri kwa matumizi ya kuber na kuitaka serikali kuingilia kati ili kudhibiti mauzo ya sigara na dawa nyingine za kulevya.

 

You can share this post!

Pasta Ng’ang’a ajuta kutisha kumuua mwanahabari

Inasikitisha serikali kuchelewesha fedha kwa maeneo kame...

adminleo