• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
FUNGUKA: ‘Nawazuga kwa maneno tu!’

FUNGUKA: ‘Nawazuga kwa maneno tu!’

Na PAULINE ONGAJI

KUNA madume wanaojipiga vifua kwamba wamebobea hasa katika kuwapanga au kuwapiga Kiswahili kina dada na kuwalaghai penzi.

Basi ikiwa wewe ni mmoja wao, basi huenda hujawahi kukutana na Belinda mwenye umri wa miaka 35 na mtaalamu wa masuala ya kifedha katika shirika moja humu nchini.

Yeye ni mama wa watoto watatu na ni mke ambapo ameolewa kwa miaka saba sasa na mumewe ni mfanyabiashara jijini Nairobi.

Biashara ya mumewe imenawiri sana kiasi cha kumchumia kitita kikubwa cha pesa kinachomwezesha kushughulikia familia yake bila tatizo lolote.

Wanaishi katika mojawapo ya mitaa ya kifahari jijini Nairobi. Watoto wao wanasoma katika mojawapo ya shule za kimataifa.

Mbali na hayo, dume hili limemnunulia mkewe gari na hulijaza mafuta na pia kugharimia mahitaji mengine yote nyumbani mwao.

Kwa hivyo unapomtazama Belinda, utadhani ni mwanadada wa kawaida aliyefanikiwa kuwa na vitu vingi ambavyo wengine walio katika umri wake hula kwa macho tu.

Mwanamama huyu ana kasoro moja. Ni mwongo ajabu hasa inapowadia kwenye mahusiano na kamwe hawezi kutosheka na mwanamume mmoja, licha ya kuwa ameolewa.

“Nimenoa kipawa changu cha kudanganya ambapo nimepanga madume kadha na wote wananiamini. Najua kwamba mimi ni mwongo ajabu ambapo kila mwanamume anayetembea nami, ni binamu yangu.

Nina wapenzi sita ikiwa ni pamoja na mume wangu na wote wanajuana, ila kila mmoja anajua kuwa mwenziwe ni binamu yangu. Hata mume wangu, machoni mwa hawa madume wengine ni binamu yangu.

Naweza kuwa na wanaume wawili katika meza moja klabuni huku kila mmoja akidhani kwamba mwenziwe ni binamu yangu.
Hata unifumanie nikimbusu kaka mwingine na wewe ni mpenzi wangu, kuna jinsi nitakavyokushawishi na kamwe hutasalia na maswali.

Kumbuka hawa ni wanaume ambao nanufaika kutokana nao kwa njia moja au nyingine. Mume wangu bila shaka ni baba wa watoto wangu na mkidhi mahitaji yetu. Kuna mwingine wa kunihudumia kimahaba, kunaye wa kunipeleka likizo za mbali na mwingine wa kunipa tu ushauri.

Kuna wakati ambapo wanaume watatu walikutana nyumbani kwangu mume wangu akiwa na cha kushangaza ni kwamba niliwaandalia chakula huku kila mmoja akidhani kwamba mimi ni wake.

Kinachofanya nibobee katika masuala haya ni kuwa kwa kawaida sionyeshi mahaba hadharani. Hata uwe mpenzi wangu sikuruhusu uniguse au hata kunishika mkono tukiwa katika maeneo ya umma.

Nina kurasa kadha za Facebook. Kila ukurasa nimeweka picha zangu na wanaume tofauti ambapo nadumisha usiri kiasi cha kuwa kila mpenzi wangu anaona ukurasa anaopaswa kuona pekee. Hakuna anayeweza kuona ukurasa ambapo nimechapisha picha zangu na dume tofauti. Isitoshe, hata hizo picha ni huyo mhusika peke anayeweza kuzitazama.

Hata kwenye mtandao wa WhatsApp ni ujanja uo huo niliotumia ambapo ni wewe pekee utakayeona picha hiyo tukiwa nawe na ukadhani sina mwingine ananikosha roho”.

You can share this post!

MWANAMUME KAMILI: Nyie mnaotangazia umma ya chumbani ni...

TAHARIRI: Wadau wafanye hima kuiokoa voliboli nchini

adminleo