• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 4:28 PM
Handisheki itawafaa Wakenya wote – Uhuru

Handisheki itawafaa Wakenya wote – Uhuru

Na VALENTINE OBARA

RAIS Uhuru Kenyatta amekosoa wanasiasa wanaopinga mwafaka kati yake na Kiongozi wa Upinzani, Bw Raila Odinga na kusisitiza hatarudi nyuma kwa ushirikiano huo.

Akizungumza Alhamisi bungeni wakati wa kutoa hotuba kuhusu hali ya taifa, Rais alisema handsheki ilikuwa ishara ya uwiano na urafiki.

Hii ni kinyume na msimamo unaoshikiliwa na Naibu Rais William Ruto na wandani wake kwamba ni njama ya Bw Odinga kumhujumu asifanikiwe kushinda urais ifikapo 2022.

“Sote tunafahamu athari mbaya tulizopitia katika miaka iliyopita kutokana na mgawanyiko baina yetu,” akasema.

Alikariri msimamo wa serikali kutenga Sh10 bilioni za kujenga sehemu za kumbukumbu kwa jamii zilizoathirika na ghasia za kisiasa.

Wakati huo huo, Rais alitangaza mpango wa kutengea sekta ya elimu fedha za kutosha katika kipindi cha kifedha cha mwaka wa 2019/2020 ili kuimarisha miundomsingi shuleni.

Shule nyingi za umma hasa za upili, zimekumbwa na changamoto mwaka huu baada ya serikali kuagiza wanafunzi wote waliofanya Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Msingi (KCPE) kujiunga na Kidato cha Kwanza. Hali hii imesababisha kuwepo wanafunzi wengi kupita kiasi shuleni.

You can share this post!

Upinzani waunga Rais mkono katika vita dhidi ya ufisadi

TAHARIRI: Maamuzi magumu yahitajika kuzima ufisadi

adminleo