• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:55 AM
Idadi ya mabao itaamua watakaotinga Nne-bora – Pochettino

Idadi ya mabao itaamua watakaotinga Nne-bora – Pochettino

NA CECIL ODONGO

MKUFUNZI wa Tottenham Hot Spurs Mauricio Pochettino amekiri kwamba vita vya kumaliza ndani ya nne bora kwenye Ligi Kuu ya Uingereza(EPL) vitaamuliwa kwa idadi ya mabao ya timu nne zinazowania nafasi hizo.

Vijana wa Pochettino wanaoshikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa jedwali la EPL, wanatenganishwa na alama nne pekee na nambari sita Arsenal ambao bado wana mechi moja ya kuwajibikia.

Akizungumza baada ya timu yake kuiaibisha Huddersfiled 4-0 katika mechi ya EPL, raia huyo wa Argentina alijishaua kwamba mabao hayo manne yatachangia Spurs kutinga nne bora na kufuzu kushiriki Klabu Bingwa Barani Ulaya mwaka wa 2019.

“Kuyafunga mabao ni muhimu sana na husaidia hatimaye. Tofauti kati ya idadi ya magoli itasaidia pakubwa wakati wa kuamua nani anamaliza ndani ya mduara wa nne bora msimu huu,” akasema Pochettino.

“Kwa kweli msimu huu mambo ni magumu na kuna ushindani mkali. Tunashindana na timu kubwa zinazopigana kumaliza katika nafasi nne bora, Klabu Bingwa Barani Uropa au kushinda Ligi Kuu ya EPL,” akaongeza mkufunzi huyo.

Klabu za Tottenham Hot Spurs, Arsenal, Chelsea na Manchester United zimejipata katika ushindani mkali wa EPL, kila moja ikilenga nne bora msimu wa 2018/19 ukielekea ukingoni.

Baada ya kushinda mabingwa watetezi wa EPL 1-0 kwenye mkondo wa kwanza wa Klabu Bingwa Barani Uropa(UEFA), Spurs wanakabiliwa na mtihani wa kutetea ushindi huo finyu kwenye kabiliano kali Jumatano Aprili 17 ugani Etihad katika mechi ya mkondo wa pili.

You can share this post!

Pogba kupokezwa ‘hongo’ ya unahodha asihamie...

Shujaa yakutanishwa na wakali Fiji na Samoa London Sevens

adminleo