• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Serikali yafufua mpango wa kufunga kambi ya Dadaab

Serikali yafufua mpango wa kufunga kambi ya Dadaab

Na Aggrey Mutambo

SERIKALI imesema itafunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab ilivyopanga awali, licha ya wakimbizi kukataa kujisajili katika mpango wa kuwarejesha mataifa walikotoka ulioanzishwa 2014.

Hii ndiyo hatua ya hivi punde zaidi ya kujaribu kufunga kambi za wakimbizi, kufuatia hofu kuwa zimekuwa zikitumiwa kama maficho ya magaidi.

Kambi hiyo iliyoko Kaunti ya Garissa imekuwa ikizungumziwa kati ya serikali, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na Somalia.

Hili ni jaribio la nne la kufunga kambi hiyo. Wakimbizi wanaonekana kukataa mpango huo. Takwimu za UNHCR zinaonyesha kuwa idadi ya wakimbizi waliorudi makwao bila kutumia mpango huo ndiyo kubwa.

Mnamo 2014, kambi hiyo ilikuwa na wakimbizi 350,000, lakini sasa idadi hiyo imepungua hadi 210,556 ambapo 202,381 wanatoka Somalia.

Takwimu za UNHCR zinasema wakimbizi 79,328 kutoka Somalia wamerejea nchini humo kupitia mpango huo. Kambi hiyo iliyoanzishwa 1991 ilikuwa na sehemu tano lakini sasa ina tatu, baada ya mbili; Kambioos na Ifo kufungwa Machi 2017 na Mei mwaka jana.

 

You can share this post!

Kaunti ya Machakos kulipa seneta Sh366 milioni

Atwoli akemea FKE kwa kupinga ushuru wa ujenzi wa nyumba

adminleo