• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
KOLERA: Mutura na mahindi choma sasa ni marufuku

KOLERA: Mutura na mahindi choma sasa ni marufuku

Na Steve Njuguna

IDARA ya Afya katika Kaunti ya Laikipia imepiga marufuku uchuuzi wa vyakula katika kaunti hiyo kufuatia ripoti za mkurupuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika sehemu kadhaa nchini.

Kwenye notisi iliyotolewa mnamo Jumatano, Kaimu Waziri wa Afya Dkt Donald Mogoi alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuzuia hali zote ambazo huenda zikasababisha ugonjwa katika kaunti hiyo.

“Kufuatia ripoti za kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu katika baadhi za sehemu nchini, Idara ya Afya imepiga marufuku uchuuzi wa vyakula katika kaunti ili kudhibiti maenezi yake,” ikaeleza notisi hiyo.

Miongoni mwa vyakula ambavyo vimepigwa marufuku ni Mutura, Soseji, Samosa, mahindi choma, mayai na mahindi ya kuchemsha.

Vyakula vingine ni mandazi, chapati, chai kati ya vingine.

Waziri alionya kuwa wale ambao watakiuka agizo hilo watakabiliwa vikali kisheria.

 

You can share this post!

Diwani ailaani serikali ya kaunti kuwanyima walemavu ajira

Madaktari waonywa dhidi ya kuanika siri za wagonjwa...

adminleo