• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 3:17 PM
Sababu za chaguzi nchini Kenya kuwa ghali

Sababu za chaguzi nchini Kenya kuwa ghali

Jumanne, Kamishna Boya Molu aliambia Kamati ya Seneti kuhusu Sheria kwamba ni hali hiyo ndiyo husababisha tume hiyo kutumia mabilioni ya fedha kununua mitambo ya kieletroniki kuendeshea shughuli za uchaguzi na kuajiri wahudumu wengi na kukodi huduma za usalama.

“Isitoshe, huu mwenendo wa kuchapishwa kwa karatasi za kupigia kura zenye alama za usalama unatokana na hali kwamba wananchi hawaamini kuwa maafisa wa IEBC wanaweza kuendesha uchaguzi huru na haki,” akasema Bw Molu ambaye alimwakilisha mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati katika kikao hicho kilichoitishwa kuchambua changamoto zilizoikumba katika uchaguzi mkuu uliopita.

Alifichua kuwa uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017, pamoja na uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika Oktoba 27, 2017, uligharimu Sh48 bilioni, akisema gharama hiyo ingepungua ikiwa “Wakenya wengekuwa watu wa kuaminiana.”

“Tulilazimika kuajiri zaidi ya makarani 4,500, maafisa wa usalama 80,000 kando na kutumia mabilioni ya fedha kununua mitambo ya kieletroniki. Isitoshe, juzi iliripotiwa magazetini kwamba IEBC ilitumia Sh700 milioni kwa siku mbili kuwalisha watu waliosimamia uchaguzi huo,” Bolu akasema.

Alitoa mfano taifa la Rwanda ambalo lilitumia Sh69 milioni katika uchaguzi wake wa 2017 kuashiria kuwa taifa hili lilitumia Sh108.5 pekee kwa kila mmoja wa wapiga kura 6.8 milioni, kutokana na imani ya wananchi kwa utendakazi wa asasi ya uchaguzi nchini humo.

“Hii ni tofauti na hapa Kenya ambapo kila mmoja wa wapigakura 14 milioni walioshiriki uchaguzi wanakadiriwa kutumia Sh25,000. Nchini Rwanda uchaguzi husimamiwa na watu wa kujitolea ambao huwa hawalipwi,” Bw Bolu akaielezea kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Nandi Samson Cherargei.

Hata hivyo, Seneta wa Siaya James Orengo alitofautiana na kauli ya kamishna huyo akisema ni wajibu wa tume hiyo kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria ili Wakenya waamini matokeo ya uchaguzi.

“Matokeo ya uchaguzi hupingwa kwa sababu ya makosa ya maafisa wa uchaguzi. Sheria ikifuatwa na vifaa vya uchaguzi vitumiwe ipasavyo suala la gharama halitakuwa na uzito wowote,” akasema.

You can share this post!

Awiti akosa kufika mbele ya Seneti kwa kuugua

Wanachama wa Urithi Housing Co-operative wahimizwa kulipa...

adminleo