• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
HUDUMA NAMBA: Usajili wakamilika wachache wakijitokeza baada ya muda kuongezwa

HUDUMA NAMBA: Usajili wakamilika wachache wakijitokeza baada ya muda kuongezwa

Na Charles Wasonga

ZOEZI la usajili wa Huduma Namba lilikamilika rasmi Jumamosi huku watu wachache wakijitokeza ishara kwamba huenda wengi watalazimika kujisajili katika afisi za machifu na manaibu wao.

Katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu foleni zilikuwa fupi katika vituo mbalimbali tofauti na hali ilivyokuwa wiki moja iliyopita kabla ya Rais Uhuru Kenyatta kuongeza muda wa usajili kwa siku saba zaidi ili kutoa nafasi kwa Wakenya zaidi kujisajili.

Mnamo Alhamisi Msemaji wa Serikali Cyrus Oguna alisema kufikia wakati huo jumla ya watu 36 milioni walikuwa wamejisajili kati ya watu 45 milioni waliolengwa.

Kwa mfano, katika kaunti ya Mandera ni watu 360,000 pekee waliokuwa wamesajiliwa kufikia Ijumaa ilhali serikali ilitarajia kuwa jumla ya watu milioni moja wangesajiliwa.

Idadi ndogo ya watu waliojitokeza kwa shughuli hiyo jana inaashiria kuwa idadi iliyolengwa haikufikiwa kumaanisha itabidi waliosalia kuenda kwa afisi za machifu kusajiliwa.

 

You can share this post!

Ruto kukosa nyama choma Amerika

Mahakama yasifiwa kwa kuharamisha ushoga na usagaji

adminleo