• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
Washukiwa wakuu sakata ya dhahabu waachiliwa kwa dhamana ya Sh1.5m

Washukiwa wakuu sakata ya dhahabu waachiliwa kwa dhamana ya Sh1.5m

Na Richard Munguti

MSHUKIWA mkuu katika kashfa ya biashara ya dhahabu feki pamoja na wenzake wawili waliachiliwa kwa dhamana ya Sh1.5 milioni pesa tasilimu baada ya kukaa rumande kwa siku saba.

Hata hivyo Bw Jared Kiasa Otieno na wenzake 15 hawakuweza kulipa dhamana walizopewa na hakimu mkuu mwendo was aa 15 alasiri.

Ilibidi warudishwe rumande hadi Jumanne jamaa wao watakapojishughulisha kulipa dhamana hiyo. Hakimu mkuu aliwaachilia washukiwa hao kwa dhamana ya viwango vitatu.

Washukiwa wengine 10 waliachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 pesa tasilimu nao raia wawili wa Congo na Chad walipewa dhamana ya Sh500milioni pesa tasilimu.

Mahakama iliwaamuru washukiwa wote wawasilishe hati zao za kusafiri kortini na wasithubutu kusafiri ng’ambo bila idhini.

Washukiwa hao waliachiliwa baada ya idara ya urekebishaji tabia kuchelewa kuwasilisha taarifa kuwahusu washukiwa 16 wanaoshtakiwa kumlaghai mfanya biashara Sh300 milioni katika kashfa ya dhahabu feki.

Hakimu mkuu Francis Andayi aliamuru washukiwa hao warudishwe rumande hadi idara hiyo ikamilishe kutayarisha ripoti hizo.

“Naomba muda kukamilisha ripoti sita zilizosalia ndipo ziwasilishwe zote mahakamani,” hakimu aliombwa na afisa wa urekebishaji tabia.

Bw Andayi aliwapa muda hadi saa kumi unusu jana wawe wamekamilisha ripoti hizo na kuziwasilisha ndipo asisome na kutoa uamuzi iwapo washukiwa hao wataachiliwa kwa dhamana.

Washukiwa hao wanaoongozwa na mfanyabiashara Jared Kiasa Odero.

Jumanne wiki iliyopita washukiwa hao walisukumwa gerezani na Bw Andayi kuwezesha maafisa wa urekebishaji tabia kuwahoji na kubaini kiwango cha dhamana wanachoweza kupata.

Miongoni mwa washukiwa hao kuna wanafunzi wawili na raia wawili wa kigeni kutoka mataifa ya Congo na Chad.

“Hii mahakama imefahamishwa miongoni mwa washtakiwa ni wanafunzi, wengine ni walinzi, wengine ni madereva wa teksi na wengine ni wafanyakazi wa nyumbani na hawawezi kupata dhamana ya juu kulingana na hali yao ya kifedha,” alisema Bw Andayi.

 

Kesi hiyo itatajwa baada ya wiki mbili.

You can share this post!

Matineja ndani miaka 30 kwa kuteka mtoto nyara na kumuua

Hofu Ziwa Victoria likinyakuliwa na wafanyabiashara

adminleo