• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 1:15 PM
Jowie kusalia ndani hadi Juni 18

Jowie kusalia ndani hadi Juni 18

Na RICHARD MUNGUTI

MPENZIWE aliyekuwa mtangazaji wa runinga Jacque Maribe, Bw Joseph Kuria Irungu almaarufu Jowie Jumanne aliwasilisha upya ombi la kuachiliwa kwa dhamana katika kesi inayowakabili ya mauaji.

Jacque na Irungu wamekanusha shtaka la kumuua Monica Kimani katika mtaa wa Kilimani mwaka 2018.

Jacque aliachiliwa kwa dhamana ya Sh1milioni ilhali Irungu alinyimwa dhamana kwa madai hana makazi yanayojulikana kwa vile “amekuwa akiishi kwa marafikize wa kike.”

Wakili David Ayuo anayemwakilisha Jowie alisema “mambo yamebadilika kwa vile jamaa wa mshtakiwa wako tayari kuwasilisha hati ya kumiliki shamba katika eneo la Nakuru.”

“Mshtakiwa hawezi kuwafikia mashahidi kwa vile wamepewa hifadhi na mamlaka ya kuwatunza mashahdi,” akasema Bw Ayuo.

Aliongeza kusema mshtakiwa hawezi kutoroka kwa vile hana pasipoti kwa vile ilichukuliwa na kuhifadhiwa na Polisi.

Akipinga hilo kiongozi wa mashtaka Bi Catherine Mwaniki alisema, “hakuna ushahidi mpya ambao umetolewa na mshtakiwa kuwezesha mahakama kubadili msimamo wake.”

Bi Mwaniki alisema mshtakiwa alimpelekea ujumbe wa vitisho nduguye marehemu Monica Kimani, siku moja kabla ya kifo.

 

Mahakama ilifahamishwa mshtakiwa yuko na kila sababu ya kutoroka kwa vile anajua akipatikana na hatia ataadhibiwa vikali.

Adhabu ya kosa linalowakabili Jacque na mpenziwe ni kunyongwa ama kufungwa jela maisha.

“Msimamo wa upande wa mashtaka ni ule ule. Mshtakiwa asalie ndani hadi kesi isikizwe na kuamuliwa. Naomba mahakama itupilie mbali ombi la mshtakiwa,” alisema Bi Mwaniki.

Jaji Wakiaga atatoa uamuzi mnamo Juni 18.

You can share this post!

Wanaume 5 kinyang’anyironi kujaza nafasi ya Njiraini...

Raia wa Kenya na Amerika ajitetea kuteuliwa balozi Korea...

adminleo