• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 6:55 AM
LEO NI LEO: Arsenal na Chelsea nani atawika Europa?

LEO NI LEO: Arsenal na Chelsea nani atawika Europa?

Na MASHIRIKA

BAKU, AZERBAIJAN

USHINDI kwa Arsenal katika fainali ya leo Jumatano dhidi ya Chelsea katika Europa League utawapa tiketi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Lakini kushindwa kwa Chelsea kutasababisha kutimuliwa kwa kocha Maurizio Sarri ambaye huu ni msimu wake wa kwanza uwanjani Stamford Bridge.

Hatua ya vinara wa ligi ya Europa kupangia fainali hiyo jijini hapa inamaanisaha kwamba klabu zote mbili zitakuwa na mashabiki wachache hasa ikizingatiwa gharama kubwa ya kuhudhuria mechi hiyo na umbali wa masafa ya usafiri.

Licha ya kusuasua katika sdehemu kubwa ya kampeni ya msimu huu, Chelsea walimaliza kipute cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika nafasi ya tatu na kufuzu moja kwa moja kwa mechi za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) muhula ujao.

Lakini kwa Arsenal waliomaliza katika nafasi ya tano, hii ndiyo njia pekee ya kuwawezesha kushiriki michuano hiyo; iwapo watatwaa ubingwa wa Europa League.

Uwanja wa Olympic Stadium unachukua watu 70,000, lakini kulingana na gharama kubwa na safari ndefu kwa mashabiki wa klabu hizi za Uingereza, huenda ukawa tu na watu 50,000. Uwanja huu unapatikana umbali wa kilomita 2,000 kutoka Moscow (Urusi) na Istanbul (Uturuki).

Arsenal na Chelsea kila moja ilipokea tiketi 7,000 kuuzia mashabiki wao walio na uwezo wa kusafiri .

Baku ni jiji tajiri kutokana na mafuta yanayopatikana kwenye visima kote jijini, na gharama ya maisha iko juu.

Mbali na kombe la Europa League, washindi wataondoka na Sh900 milioni, mbali na mgao mwingine kutokana na matangazo ya kusambaza habari za mechi hiyo.

Manchester United ilikuwa klabu ya mwisho kutoka Uingereza kutwaa ubingwa wa Europa League mnamo 2016 – ambapo ilipokea jumla ya Sh5 bilioni.

Chelsea walitinga fainali kufuatia ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Eintracht Frankfurt kupitia kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 katika mikondo yote miwili, hatua ya nusu-fainali.

Penalti

Kipa wao, Arrizabalaga aliokoa penalti za Martin Hinteregger na Goncalo Paciencia wakati wa matuta hayo, huku mkwaju wa Casar Azipilicueta wa Chelsea ukunyakwa na kipa Kevin Trapp wa Frunkfurt.

Kwenye nusu-fainali nyingine, Arsenal iliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 7-3 dhidi ya Valencia baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kufunga mabao matatu katika mechi ya marudiano katika ushindi wao wa 4-2 ugenini katika mechi nchini Uhispania.

“Tulitatizika katika mkondo wa pili baada ya kuondoka kwa Andreas Christensen na Ruben Loftus-Cheek, na hatukuwa na watu sawa wa kujaza nafasi hizo,” alisema kocha wa Chelsea, Sarri.

Kwa upande wake, Unai Emery alisema vijana wake wako tayari kwa pambano la leo ambalo anatarajiwa kuwategemea Aubameyanga na Lacazette.

You can share this post!

Utumiaji wa mihadarati haufai kuwa kosa – Sabina Chege

MAPISHI: Mandazi

adminleo