• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 4:25 PM
Wanafunzi wahamasishwa kuhusu upandaji miti

Wanafunzi wahamasishwa kuhusu upandaji miti

NA RICHARD MAOSI

Wanafunzi kutoka shule ya wavulana ya Jomo Kenyatta katika eneo la Bahati kaunti ya Nakuru, wamepanda miche 1,000 kuadhimisha siku ya Madaraka Dei.

Hafla hiyo iliwaleta pamoja wanafunzi wa vyama viwili yaani kile cha kulinda mazingira na wale wa kutoa ushauri nasaha.

Miche hiyo ilipandwa katika uwazi unaozunguka shule,na kufikia mwendo wa saa tano asubuhi zaidi ya miti 400 ilikuwa imepandwa.

Kulingana na naibu mwalimu mkuu Bw George Macharia aliyeongoza shughuli hiyo alisema,hiyo ilikuwa ni njia ya kuwahimiza wanafunzi waboreshe mazingira.

Alieleza kuna manufaa kama vile kuzuia udongo wenye rotuba usibebwe na maji,na kufanya hivyo tutakuwa tumehifadhi maji yaliyo ndani ya udongo.

Mwalimu Macharia alisema zaidi ya miche 300 iliyopandwa, inaweza kustahimili ukame akisema miti ina faida nyingine kama vile kuvuta mvua..

Zoezi hilo lililoanza mwendo wa saa mbili asubuhi lilijumuisha upanzi wa aina mbalimbali ya miche na baadae wakanyunyizia maji mwishoni mwa shughuli.

“Tunawashukuru wanafunzi wetu kwa kujitokeza kuunga mkono hatua ya kupanda miti,isitoshe tunawahimiza wajiandae kwa shughuli nyinginezo kama hizi baadae,”Macharia alisema.

Mwalimu Macharia alipongeza idara inayosimamia misitu KFS (Kenya Forest Service) tawi la Nakuru kwa kugharamia miche shughuli ya kupanda miti inapotokea.

Mnamo Machi msimamizi wa uhifadhi wa msitu wa Mau katika Bonde la ufa Fred Ogombe alieleza Taifa Leo kuwa, kaunti imeweka mikakati ya kushirikiana na wawekezaji wa kibinafsi pamoja na umma kufikisha asilimia 10 inayohitajika.

You can share this post!

Miamba wa soka duniani

ODM wapinga noti mpya

adminleo