UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Sifa za mkufunzi, mwanagenzi katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili
Na MARY WANGARI
ILI kufanikisha mchakato wa ufundishaji wa lugha ni muhimu kwa mkufunzi kudhihirisha sifa zifuatazo:
i. mkufunzi anapaswa kuwa mwasilishaji mzuri
ii. awe na utaratibu na mpangilio wa kiwango cha juu
iii. ni muhimu awe mstahimilivu
iv. ni sharti awe na ujuzi wa kufundisha
v. anafaa kuwa na uhusiano mzuri na wanagenzi
vi. anastahili kuwa na maarifa kuhusu somo husika.
Pamoja na hayo mwanagenzi anayejifunza lugha anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
i. ni sharti awe tayari kujifunza lugha ya Kiswahili bila kulazimishwa
ii. anapaswa kufanya mazoezi mara kwa mara ya kuitumia lugha hiyo
iii. ni sharti awe na maarifa ya kumwezesha kupambanua dhana mbalimbali ili kugundua mambo ambayo jamii fulani inayafanya
iv. anafaa awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo
v. ni muhimu awe na ratiba ya kujifunza
vi. anastahili kulinganua na kulinganisha lugha anayojifunza
vii. mwanagenzi anafaa kuwa na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii husika
viii. ni sharti awe mtendaji
ix. mwanagenzi hana budi kuzingatia ubora ili aweze kujifunza zaidi.