• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:24 AM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Jinsi ya kufundisha darasa mseto

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Jinsi ya kufundisha darasa mseto

Na MARY WANGARI

NI sharti kama mwalimu uwe na maarifa kuhusu tamaduni na itikadi za wanajamii mbalimbali kama vile Wazungu, Wachina, Waarabu na kadhalika.

Ili kufanikiwa katika ufundishaji wa darasa mseto, ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:

Ni sharti uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kwa mfano, kama ni lugha ya Kiswahili basi pendelea kutumia Kiswahili ili usiwakwaze sana. Hata hivyo lazima wawe na lugha ambayo wewe unaijua

Tumia vitendo halisi, mathalani ishara na kadhalika.

Toa mwaliko kwa wageni mbalimbali ili waje waeleze kuhusu lugha na mazingira.

Wakati mwingine utahitajika kupuuza malengo ya wanafunzi.

Zingatia kwamba ufundishaji wa masuala ya utamaduni ni sharti ufungamane na muktadha husika.

Sifa za mpataji lugha

Mpataji lugha ni lazima awe na sifa kuu mbili ambazo ni:

1. Umilisi wa kiisimu

Huu ni uwezo alio nao mtu anayejifunza lugha ambao unamwezesha kutofautisha viambo, miundo tofauti ya lugha na msamiati wa lugha

Aidha, ni kuwa na uwezo wa kuitamka lugha ile.

2. Umilisi wa kiisimujamii

Hii ni aina ya umilisi wa lugha ambapo mtumiaji wa lugha hupata lugha inayomwezesha kujifunza lugha na kuzingatia muktadha.

 

Nadharia, mbinu na mikabala husika katika kujifunza lugha ya pili

Dhana ya nadharia inarejelea mkondo wa mawazo unaotumika kuelezea jambo fulani.

Kwa mujibu wa Mtesigwa (2009), nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo au vitendo vinavyohusisha uchunguzi, mpangilio na uchanganuzi wa matukio katika kukabili suala fulani kisayansi. Kwa mintarafu hii, ni vyema tutilie maanani mambo haya mawili:

Njia za ufundishaji lugha ya kigeni ni tele sawia na walimu walivyo wengi.

Zingatia hali ya darasa. Tumia njia au mbinu zaidi ya moja darasani. Usitumie njia moja tu.

Kwa upande wao Rogers & Richards (2001), wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda kufundisha tunahitaji kujiuliza maswali yafuatayo:-

  1. Malengo ya ufundishaji lugha lengwa (LL) ni yapi? Mfano labda lengo lao linaweza kuwa wanataka kuzungumza tu.
  2. Msingi asili wa lugha lengwa ni upi na unaathiri vipi njia za kufundisha. Mfano kaida za lugha ya Kiswahili ni zipi?
  3. Ni misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?
  4. Ni misingi ipi ya upangiliaji wa mada? Kwa mfano, kwa kuzingatia suala la utamaduni mathalani salamu na kadhalika.
  5. Je, lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza lugha? Mfano; miundo ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?
  6. Je wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha hiyo?
  7. Je ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya pili au ukipenda lugha ya kigeni.

 

[email protected]

Marejeo

Msanjila, Y. P. (1990). “Problems of Teaching Through the Medium of Kiswahili in Teacher Training Colleges in Tanzania”. Journal of Multilingual and Multicultural Development II/4:307 – 318

Mtembezi, I. J. (1997). Njia Mbili Zilimshinda Fisi: Tanzania na Suala la Lugha yaKufundishia. Dar es Salaam: BAKITA.

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Muktadha wa ufundishaji lugha;...

MAPOZI: Mary Oyaya

adminleo