• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Kenya yarahisisha mchakato wa uhamiaji

Kenya yarahisisha mchakato wa uhamiaji

Na BERNARDINE MUTANU

Kenya imo katika nafasi ya tisa Afrika kati ya mataifa ambayo ni rahisi kwa wageni kuzuru katika viwango vya mataifa yaliyo na sera wazi kuhusu visa.

Viwango hivyo ambavyo huchapishwa na Benki ya African Development (Afdb), vinaonyesha Kenya imepanda kutoka nambari 15 mwaka wa 2017 hadi nambari tisa mwaka wa 2018.

Benki hiyo ilieleza kuwa kuimarika kwa Kenya kumetokana na agizo la Rais Uhuru Kenyatta la 2017 la kutopewa viza kwa raia kutoka Afrika punde wanapofika nchini, katika viwanja vyovyote wanavyoingilia.

“Kenya iliimarika kwa nafasi sita kuwa kati ya mataifa 10 bora katika utoaji wa viza,” ilisema AfDB katika taarifa.

Mataifa ya Seychelles, Benin na Rwanda, ambayo yalikuwa nambari moja, mbili na tatu kwa mfuatano huo, pia yana sera wazi ya utoaji wa viza kwa raia wote kutoka barani Afrika.

Mataifa nane ya mwanzo katika orodha hiyo katika eneo la Afrika Mashariki ni Comoros, Djibouti, Kenya, Rwanda, Seychelles, Somalia, Uganda na Tanzania.

Ni vigumu kwa wageni kuingia katika mataifa yaliyoko eneo la magharibi mwa Sahara na kufuatwa na Equatorial Guinea naSudan.

Orodha hiyo hutolewa kwa lengo la kuonyesha ni mataifa yepi Afrika ambayo ni rahisi kupata viza kwa kuangalia matakwa ya kuingia nchini kwa mataifa mengine Afrika wanaposafiri.

You can share this post!

Serikali yatoa magunia 600,000 kupunguza bei ya unga

Rekodi muhimu kuhusu Sharon na Melon zakosekana hospitalini

adminleo