Huenda Boinnet na Kihalangwa wakatupwa ndani
Na RICHARD MUNGUTI
INSPEKTA Jenerali wa Polisi Joseph Boinnet na Mkurugenzi wa Idara ya Uhamiaji Gordon Kihalangwa wanaweza kusukumwa ndani wakati wowote baada ya Mahakama ya juu kukataa kutupilia mbali maagizo wawili hawa waadhibiwe kwa kukaidi maagizo ya korti.
Wawili hawa wanaweza kusukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani.
Majaji Roselyn Nambuye, Kathurima M’Inoti na Patrick Kiage walisema wakuu hao wa Serikali walikaidi agizo la Jaji Luka Kimaru la kumfikisha mwanaharakati Miguna Miguna kortini.
Badala ya kumfikisha kortini , Bw Kihalangwa alimsafirisha Bw Miguna hadi Canada akidai ni mhamiaji haramu.
Majaji hao watatu walitupilia mbali rufaa aliyowasilisha waziri wa usalama Dkt Fred Matiang’I iliyopania kuwatoa kwenye ndoano Boinnet na Kihalangwa.
“Hii mahakama haiwezi kukubalia wakuu serikalini kukaidi maagizo ya mahakama hata iweje,”majaji Nambuye, M’Inoti na Kiage walisema.