• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
Wezi watumia misongamano kupora vipuri vya magari jijini

Wezi watumia misongamano kupora vipuri vya magari jijini

Na AMOS NGWOMOYA

WIZI wa vipuri vya magari umechukua mkondo wa aina yake huku wezi wakilenga waendeshaji magari katika msongamano wa trafiki.

Gazeti la Daily Monitor limebaini kwamba uhalifu huo haufanyiki tu katika barabara zinazoathiriwa mara kwa mara na trafiki jijini kama vile Entebbe Road lakini pia katika barabara nyingine zenye shughuli nyingi viungani mwa jiji.

Kutoka uhalifu wa kawaida wa kuwapokonya waendeshaji simu na vifaa vinginevyo, majambazi hao ambao tumegundua huwa wanaenda wakiwa wawili wawili, hung’oa vioo vya upande wa magari na kutoroka.

Mwendeshaji gari aliyezungumza na Daily Monitor wiki iliyopita baada ya kioo chake kung’olewa alisema uhalifu huo unaongezeka kwa kasi sana.

“Nilikuwa nikiendesha gari aina ya Toyota Premio na kulikuwa na msongamao mkubwa wa magari. Vijana wawili niliofikiria walikuwa wapita njia waliibuka kutoka Barabara ya John Ssebaana Kizito na walipofika kwenye gari langu waling’oa kio cha upande cha gari langu na kutoweka. Niliachwa bila kujua la kufanya kwa sababu sikuona walikoelekea,” alisema Ismael Senoga anayejihusisha na biashara ya kuuza vifaa vya ujenzi katika Dastur Street. Bw Senoga alisema maafisa wa usalama wanapaswa kuwasaka majambazi hao wanaopiga kambi katika barabara za jiji ili kuwashambulia waendeshaji magari.

Mwanahabari alizungumza na waendeshaji magari kadha katika Entebbe Road waliothibitisha wizi huo.

Uhalifu wa kawaida

Baadhi ya waendeshaji pikipipiki ambao kituo chao kiko kando na Clock Tower, walifichua kwamba uhalifu huo ni wa kawaida hasa kati ya saa mbili na saa tatu jioni.

Walisema pia wahuni hao huwa wamejihami kwa vyuma ambavyo hutumia kung’oa vioo vya gari kabla ya kutoweka kuelekea Nakivubo Channel ambapo ni nadra wao kufuatiliwa.

Inashangaza kuwa wanawahangaisha waendeshaji magari machoni pa maafisa wa trafiki ambao, kulingana na kazi yao, wanashindwa kuwafuatilia wahalifu hao huku wakidhibiti trafiki.

Msemaji wa Kampala Metropolitan Police, Patrick Onyango alisema polisi tayari wametuma vikosi katika maeneo yanayokumbwa na msongamano wa trafiki.

  • Tags

You can share this post!

SHANGAZI AKUJIBU: Mke ataka tulishane mahaba tu, anikataza...

SEKTA YA ELIMU: Wazazi wafurahia nafasi ya kubadilisha...

adminleo