• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
SIHA NA LISHE: Epuka vyakula hivi mara kwa mara kwa ajili ya afya bora

SIHA NA LISHE: Epuka vyakula hivi mara kwa mara kwa ajili ya afya bora

Na MARGARET MAINA

[email protected]

“WEWE ni kile ambacho unakila.”

Hii inamaanisha kuwa mwonekano wetu na afya ya miili na akili unajengwa na vyakula tunavyovila.

Madhara ya baadhi ya vyakula yamejengeka kwa msingi kwamba huzeesha ngozi kwa haraka na haina budi kuvijua na kuviepuka.

Vyakula hivi japo tunavipenda sana lakini vina athari mbaya kwa miili yetu na ni muhimu kujifunza tabia ya kuviacha katika milo yetu.

Kama si rahisi kuacha kabisa, basi angalau tunashauriwa kupunguza matumizi yake.

Nyama nyekundu

Mojawapo ya vyakula vinavyozeesha ngozi ni nyama hasa nyama nyekundu. Nyama nyekundu kutoka kwa mifugo kama ng’ombe, mbuzi, kondoo na kadhalika, ni mbaya kwa afya bora ya binadamu na kwa ngozi pia.

Nyama nyekundu ina kemikali aina ya carnitine ambayo inafanya mishipa ya damu kukakamaa na kusababisha kuzeeka kwa ngozi. Hivyo basi ni muhimu kupunguza ulaji wa nyama aina hii.

Chumvi

Chumvi hasa yenye madini ya iodine ni mbaya sana kwa afya ya ngozi ikiliwa mbichi. Inasababisha chembechembe za nyama katika ngozi kuvimba.

Sukari

Sukari japo tunaipenda sana, ni adui mkubwa wa afya ya binadamu.

Inadhoofisha mfumo wa kinga za mwili.

Kiasi kingi cha sukari mwilini kinafanya ngozi kuwa kavu na kufanya mwili utengeneze makunyanzi kwa sababu inaharibu kemikali ya collagen na elastin ambazo zinafanya kazi ya matunzo ya ngozi kwa kuifanya isiharibike na kuwa chakavu.

Sukari nyingi inasababisha mwili kukosa nguvu ya kupambana na bakteria. Ongezeko la bakteria hawa kunafanya utengenezwaji wa kemikali mbaya ambazo husababisha uchakavu wa ngozi.

Watu wanashauriwa kutumia sukari asilia kama ya matunda na asali kuliko zile zinazopatikana katika vinywaji kama soda,biskuti au vitafunwa vingine vyenye sukari ya kuongeza.

Vyakula vya kukaangwa

Vyakula vya kukaangwa kama chipsi, nyama ya kukaanga, husababisha uingizaji wa mafuta mengi mwilini.

Mafuta haya yana ‘Free Radicals‘ zinazosababisha uzibaji wa vinywelea katika ngozi.

Mafuta mengi mwilini yanasababisha madhara mengi mengine yakiwemo magonjwa ya moyo na kisukari.

Mkate mweupe, tambi na keki

Vyakula hivi vina kemikali ya glucemic kwa kiwango kikubwa na ambayo inaleta madhara yakiwemo magonjwa ya ngozi.

Pombe

Unywaji wa pombe unasababisha mnywaji kupoteza maji mengi mwilini kwa njia ya mkojo na huleta madhara mabaya kwa ngozi kwa kuifanya iwe kavu.

Kahawa (Caffeine)

Kemikali ya caffeine iliyo katika kahawa na vinywaji vingine husababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi na kuifanya iwe kavu. Lakini pia caffeine inasababisha utengenezwaji wa kemikali ya cortisol ambayo inachangia ngozi kuzeeka.

You can share this post!

Madagascar tayari kwa mtihani wa Tunisia katika 8-bora

Babeli ya Uhuru

adminleo