• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
Miaka 50 tangu binadamu kutua mwezini

Miaka 50 tangu binadamu kutua mwezini

 Na AFP

WASHINGTON, AMERIKA

ULIMWENGU Jumapili uliadhimisha miaka 50 tangu ziara ya kwanza kwenye mwezi kufanywa, maelfu kutoka pembe tofauti za dunia wakisherehekea.

Hii ni kufuatia tukio la usiku wa Julai 20, 1969 ambapo raia wa Amerika Neil Armstrong aliweka historia kama binadamu wa kwanza kukanyaga na kutembea katika mwezi.

Shirika linaloshughulika na mambo ya angani na utafiti wa kisayansi (Nasa) liliadhimisha siku hiyo, likipeperusha video za jinsi Armstrong aliingia mwezini moja kwa moja kwa walimwengu kujionea.

Kifaa cha kisayansi kilichoenda katika mwezi 1969 kilifika eneo liitwalo Tranquility Base. Amrstrong alikuwa amesafiri na wenzake Buzz Aldrin na Michael Collins, wote ambao walizaliwa 1930.

Wawili hao bado wako hai, japo Armstrong aliaga dunia mnamo 2012, alipokuwa na umri wa miaka 82. Aldrin ndiye alikuwa wa pili kukanyaga mwezini, naye Michael Collins akawa wa tatu.

You can share this post!

Viongozi wapinga uuzaji wa viwanda vya sukari

Gor na Bandari wafahamu wapinzani wao Klabu Bingwa Afrika

adminleo