• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 2:13 PM
Familia yapigania mwili wa aliyekufa kwa Ebola

Familia yapigania mwili wa aliyekufa kwa Ebola

Na AFP

KIZAAZAA kilizuka katika wilaya ya Kikuube, Uganda, pale jamaa wa mtu aliyeshukiwa kuambukizwa Ebola walijaribu kuuchukua mwili wake kutoka kituo cha afya.

Kwa mujibu wa maafisa wa afya, Jawiya, 34, mkazi wa Kituo cha Senjojo, parokia ya Buhuka kaunti ya Kyangwali, alifariki Jumamosi usiku jamaa zake walipokuwa wakimpeleka katika kituo cha afya cha Buhuka.

Walioshuhudia kisa hicho walisema jamaa zake waliitisha mwili wake kwa shughuli ya mazishi, lakini maafisa wa afya wakakataa kuutoa kwa sababu hawakuwa na mavazi ya kujikinga wala ujuzi wa kuwazika wahasiriwa wa Ebola.

Hata hivyo, jamaa walivamia kituo hicho cha afya, wakachukua mwili na kuusafirisha katika kituo cha Nsonga kabla ya kurejeshwa.

“Kikosi cha usalama kiliwasimamisha jamaa wa Nsonga walipokuwa tayari wameuweka mwili kwenye meli tayari kuanza safari kuelekea kituo cha Senjojo,” alisema Bw Original Okumu Ngamita, mwenyekiti wa Parokia ya Buhuka.

Alisema familia ya marehemu ilijaribu kupinga hatua hiyo, lakini maafisa wa usalama walizima injini ya meli na kuizuia kungo’a nanga.

“Tuliwashauri washirikiane na kukubali maafisa wa afya kumzika jamaa wao wakitumia mavazi ya kujikinga kwa sababu alikuwa na dalili sawa na zile za ugonjwa wa Ebola,” alisema afisa wa afya aliyechelea kutajwa.

Ripoti zilisema kwamba, marehemu alikuwa amesafiri katika Demokrasia ya Congo wiki mbili zilizopita na aliporejea Uganda, akaanza kuwangwa na kichwa, kuendesha na mafua bila kikomo.

Alitibiwa kwa ugonjwa wa Malaria katika zahanati ya kibinafsi lakini afya yake ikazidi kuzorota.

“Mnamo Jumamosi, alianza kutokwa damu kupitia mdomo na puani. Kwa bahati mbaya, alifariki njiani alipokuwa akipelekwa katika kituo cha afya,” alisema Dkt Nicholas Kwikiriza, afisa wa afya wilayani humo.

Kwingineko, Waziri wa Afya katika taifa la Demokrasia ya Congo alijiuzulu Jumatatu, akitaja kuondolewa kwake kama kiongozi wa kikosi cha kuangazia Ebola na wasiwasi kuhusu “jaribio” jipya lililopendekezwa kupitia chanjo mpya ambayo haijaidhinishwa.

“Kutokana na uamuzi wako wa kuweka shughuli ya kuangazia mkurupuko wa Ebola chini ya usimamizi wako moja kwa moja, nimewasilisha barua kujiuzulu kama waziri wa afya,” ilisema barua ya kujiuzulu ya Oly Ilunga kwa Rais Felix Tshisekedi.

You can share this post!

Migne ataka Stars kuwa macho dhidi ya Tanzania CHAN

Ulevi wa wanawake wachambuliwa

adminleo