• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Wakili kizimbani kwa kupungukiwa na hela

Wakili kizimbani kwa kupungukiwa na hela

Wakili Robert Githaiga akiwa kizimbani katika mahakama ya Milimani Machi 19, 2018 alipokana shtaka la kupeana hundi akijua fika kuwa hakuwa na pesa za kutosha katika akaunti yake. Picha/Richard Munguti

Na RICHARD MUNGUTI

WAKILI mmoja  jijini Nairobi alijipata pabaya Jumatatu aliposhtakiwa kwa kutoa hundi ya kuilipa kampuni ya magari akijua hakuwa na pesa za kutosha katika akaunti yake.

Alishtakiwa kwa kujifanya alikuwa na uwezo wa kulipa na kukosa pesa za kutosha kulipa hundi aliyoandika.

Robert Githaiga aliomba ahurumiwe na hakimu mkuu Francis Andayi na kuachiliwa kwa dhamana.

“Mimi ni wakili na naomba nionewe huruma. Naomba hii korti isinipe kiwango cha juu cha dhamana. Sitatoroka,” Bw Githaiga akaililia mahakama.

Wakili huyo alishtakiwa mnamo Feburuari 28, 2018 kwa kuipa kampuni ya kuuza magari ya Prime Cars  hundi ya Sh130,000 akijua hana pesa za kutosha katika akaunti yake ya benki.

Bw Andayi alimwachilia kwa dhamana ya pesa taslimu Sh50,000.

Aliorodhesha kesi kusikizwa Aprili 23.

You can share this post!

Timu ya Riadha ya Kenya yapokelewa kishujaa JKIA

Mahakama yaagiza Kenya Re isiteue mkurugenzi mpya

adminleo