Mahakama yaagiza Kenya Re isiteue mkurugenzi mpya
Na RICHARD MUNGUTI
MAHAKAMA ya kuamua mizozo ya wafanyakazi na waajiri imesimamisha mipango ya kumteua meneja mkurugenzi mpya wa shirika la Kenya Re.
Jaji Byram Ongaya aliamuru Kenya Re isithubutu kumteua afisa mwingine kuchukua mahali pa Bw Jadiah Mwarania.
Pia Jaji Ongaya aliamuru shirika hilo lisitangaze nafasi ya kazi ya MD hadi kesi aliyowasilisha Bw Mwarania isikizwe na kuamuliwa.
Katika kesi iliyowasilishwa na wakili Judith Guserwa , Bw Mwarania anasema amelihudumia shirika hilo kwa muda wa miaka 27 na hatua ya kumtimua kazi ilikaidi sheria za uajiri.
Jaji Ongaya alimwamuru Bi Guserwa awakabidhi washtakiwa nakala za kesi hiyo aliyoiorodhesha kusikizwa Machi 20.
Bw Mwarania alisema katika taarifa yake ya kiapo kwamba kutumiliwa kazini kwake kulitokana na kutekelezwa kwa maagizo ya mkuuu wa utumishi wa umma kwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi